Wafrika 10 mashuhuri wanaovuma kwenye mitandao ya kijamii

facebook
facebook

Wafrika hupenda sana kufuatilia matukio muhimu duniani yakiwemo kuiga  na kufurahia mafanikio ya wale ambao wanaonekana kama vielelezo maishani mwao. 

Hapa Kenya, tunapenda sana kufuatilia mafanikio yao ya kila uchao katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Watu hao wameibukia kwa kufanya mambo ya kipekee ambayo hutupa raha, kutumotisha, kuelimisha na hata kuburudisha. Wafuatao ni watu mashuhuri wakiwemo wanasoka, wasanii na waigizaji wanaovuma sana barani Afrika.

Lupita Nyong’o

Mshindi wa tuzo la uigizaji la Oscar, Lupita Nyong’o, ni miongoni mwa waigizaji bora zaidi wanaofuatiliwa sana katika mitandao ya kijamii. Luptia Nyong'o ana wafuasi zaidi ya milioni 8.1.

Diamond Platinumz

Msanii huyu wa miziki ya 'Bongo Flavour' ana wafuasi zaidi ya milioni 7.8 katika mtandao wa Instagram.

 

Akon

Nyota huyu wa kimataifa ni raia wa Senegal. Ana zaidi ya wafuasi milioni 6.3.

Mohamed Salah

Mwanasoka huyu kutoka Misri anachezea ya Liverpool katika ligi  kuu ya Uingereza. Ana wafuasi zaidi ya milioni 32.8.

Zari Hassan

Zari ni mjasiariamali mashuhuri. Ana  wafuasi milioni 6.4 katika Instagram.

Trevor Noah

Mchekeshaji huyu kutoka Afrika kusini anazaidi ya wafuasi milioni 4.9 Instagram.

Wizkid

Wizkid ni msanii wa kimataifa. Ni raia wa Nigeria huku akiwafuatwa na zaidi ya  mashabiki milioni 8.4 mtandaoni.

Samuel Eto`o

Nyota huyu wa soka anatoka katika taifa la Cameroon. Anawafuasi zaidi ya milioni 3.6 kwenye Instagram.

Eric Omondi

Mchekeshaji huyu kutoka Kenya anashabikiwa na watu zaidi ya milioni 2.2 kwenya Instagram

French Montana

Huku akifuatwa na zaidi ya watu millioni 12 mitandaoni, msanii huyu kutoka Morocco amewavutia mashabiki wengi sana.