Wakenya 184 wamepatikana na virusi vya corona nchini- Rashid Aman

Eatw-C2X0AAX1vP.jfif
Eatw-C2X0AAX1vP.jfif
Katika kikao cha kila siku kwa taifa kuhusiana na virusi vya corona nchini,katibu msimamizi katika wizara ya afya Dr Rashid Aman amesema watu 184 wamepatikana na virusi hivyo hatari.

Kutokana na takwimu hizo mpya sasa Kenya ina wagonjwa 4044 walioambukizwa corona.

Wanaume ni 129 huku wanawake wakiwa 55.

Nairobi ina 111 ,Mombasa 19,Kajiado 14 Meru 13 ,Busia 6.,Nakuru 4,Machakos 3,Kwale 1,Kisumu 1,Garrissa 1,Taita Taveta 1,Vihiga 1.

Kufikia sasa majimbo 40 yameandikisha visa hivyo vya corona.

Watu 27 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha watu 1,354 waliopona.

Wagonjwa wawili wamefariki na kufikisha watu 107 waliofariki.

Visa vipya vilivyosajiliwa katika kaunti ya Busia vimetokana na madereva wa malori waliofanyiwa vipimo.

Aman amesikitikia idadi kubwa ya vifaa gushi vya kupima virusi hivyo nchini akisema ni sharti serikali sasa ianze kupiga msasa katika maduka majula yanayoendelea kuwauzia wakenya vifaa hivyo.

Amesema ni sharti watu wafanyiwe vipimo katika vituo vilivyodhibitishwa na serikali.