Wakenya watatu ni miongoni mwa watu 26 waliouwa katika shambulizi la kigaidi katika hoteli moja huko kismayu nchini Somalia . Rais wa jimbo la Jubaland Ahmed Madobe amesema shambulizi hilo pia liliwajeruhi watu 56 .Tanzania pia imewapoteza raia wake watatu .wengine ni raia wawili wa amerika ,moja wa Canada na muingereza mmoja .
Mkusanyiko wa Habari na matukio muhimu ..
Mmarekani mbakaji akamatwa
Waendesha mashtaka nchini marekani wame mkamata mwanamme mmoja kutoka jimbo la Pennsylvania kwa kuwadhulumu kimapenzi wasichana wanne wadogo katika makaazi ya kuwalinda watoto katika kaunti ya bomet . mshukiwa Gregory Dow mwenye umri wa miaka 60 alitekeleza dhulma hizo katika makaazi alioznsiaha kuwapa hifadhi watoto mwaka wa 2017 .Atafikishwa kortini Ijumaa wiki ijayo .
Wakimbizi wazuia jitihada za Kenya kuangamiza Polio
Kenya inaweza kuangamiza kabisa polio endapo itafuata ratiba ya chanjo dhidi ya virusi vya ugonjwa huo .Mtaalam wa matibabu Fredrick Kairithia hata hivyo anasema kuingia nchini kwa wakimbizi ambao nchi zao hazina mipango ya chanjo kunafanya kuwa vigumu kenya kuafikia hilo .
Waiguru afunga ndoa na kipenzi Waiganjo
Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru jana alifunga ndoa ya kitamaduni na mpenziwe wakili kamotho waiganjo . Harusi hiyo ilifanyika katika shule ya msingi ya Kiamugumo kwenye hafla iliyohudhuriwa na rais uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga .
Wakaazi 3000 Magarini waachwa bila makao
ZAidi ya wakaazi 3000 wa Kadzuhoni katika eneo bunge la magarini wameachwa bila makao baada ya nyumba zao kubomolewa na mstawishaji wa kibinafsi . mbunge wa eneo hilo Michael Kingi amesema ingawaje korti ilikuwa imetoa agizo la kumpa ruhusa msatawishaji huyo ruhusua ya kuwaondoa wakaazi kutoka shamba hilo,wenyeji hao walikuwa tayari wamekata rufaa dhidi ya uamuzi huo na kesi hiyo ingesikizwa tarehe 22 mwezi huu .
Jamaa aliyemuua jirani yake akamatwa
Polisi huko Kericho wanamzuilia mshukiwa mwenye umri wa miaka 25 anayedaiwa kumwua jirani yake kwa kumkata kichwa na kuwajeruhi watu wengine wawili sieku ya ijumaa usiku . Mshukiwa Denis Korir alikamatw akatika kituo cha kibiashara cha Sossiot akitoroka .
Utalii utaimarika mwaka huu
Sekta ya utalii inataraji kuboreka kwa shughuli za utalii mwaka huu kuliko ilivyokuwa mwaka jana . maneja mkurugenzi wa HOteli ya Diani Reef Bobby Kimani amesema ingawaje kuna upungufu wa asilimia moja wa idadi ya watalii wanaowasili nchini ,kuna uwezekano wa idadi hiyo kuongezeka kwa ajili ya kuwepo kwa mashrika mengi ya kufanikisha safari za utalii kutumia mtandao .
Mwanahabari mashuhuri Somalia Miongoni mwa waliouawa jana
Takriban watu 26 akiwemo mwanahabari mashuhuri wa Somalia na raia kadhaa wa kigeni wameuawa katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa katika hoteli moja mjini kismayu kusini mwa Somalia . mlipujia wa kujitoa mhanga alilielekeza gari lililojaa vilipuzi katika hoteli hiyo na kisha baadaye wapiganaji waliojihami kuanza kuwafyatulia watu risasi katika hoteli hiyo .mwanahabari Hodan Nalayeh mwenye umri wa miaka 43 na mumewe Farid ni miongoni mwa waliouwa . wakenya watatu pia waliaga dunia katika shambulizi hilo.
Msipeleke mzozo wa ugavi wa mapato kortini,Ruto awaambia magavana
NAIBU wa rais William Ruto amewahimiza magavana na maseneta kutowasilisha mzozo wa ugavi wa mapato kortini na badala yake kujadiliana na serikali na bunge kumaliza utata huo . Wito wake huo unajiri wakati magavana na maseneta wanapojitayarisha kufanya maandamano kesho hadi bungeni ili kulalamikia utata kuhusu mswada wa ugavi wa mapato unaochelewesha kutolewa kwa pesa za kaunti .
Team Wanjiku Mombasa
Gavana wa Nairobi Mike Sonko ataongoza kundi la Team wanjiku kwa mkutano wa hadhara huko Mombasa . Mkutano huo utafanyika katika uwanja wa Aldina katika eneo bunge la Jomvu. Mbunge wa gatundu kusini moses kuria ,mbunge EALA Simon Mbungua ,wabunge wa zamani kalembe ndil na Reuben Ndolo pia watahudhuria mkutano huo.
Joyce Akinyi akamatwa na Heroine
Mfanyibiashara Joyce Akinyi alikamatwa jana na Polisi mtaani Nairobi west akiwa na kilo mbili za heroine . Akinyi alikamatwa pamoja na raia mmoja wa Congo na watafikishwa kortini hapo kesho .
Walimu wanafaa kupandishwa vyeo mara moja-knut
Muungano wa walimu Knut sasa unataka walimu elfu 50 kupandishwa vyeo mara moja baada ya uamuzi wa mahakama wa siku ya ijumaa ambao unaitaka tume ya TSC kutumia utaratibu mpya wa kuwahamisha na kuwapandisha vyeo walimu ili kuendeleza pia taaluma zao . Katibu mkuu Wilson Sossion amesema TSC inafaa kujadiliana kwa haraka na bunge ili kutengewa fedha za kuwapandisha vyeo walimu hao.