Wakenya wanakuombea rais! Usemi wa naibu rais William Ruto

EZavqfCWAAAPnNu.jfif
EZavqfCWAAAPnNu.jfif
Wakenya wanakuombea rais! Ni usemi wa naibu wa rais William Ruto katika maadhimisho ya siku ya Madaraka yaliyokuwa yanafanyika katika Ikulu ya Nairobi. Ruto amesema virusi vya corona ulimwenguni vimefanya watu kuwajibikia usalama wao baada ya watu wengi kuathirika na wengine kupoteza maisha.

"In fact the pandemic has made everybody realise our inadequacy and what God can do," amesema Ruto

Ruto aidha amesikitikia hatau ya makanisa kufungwa, shule kufungwa, wakenya kuendelea kupoteza ajira na hata baadhi ya biashara kufungwa kutokana na virusi hivyo hatari.

"Churches are shut, Kenyans have had to leave jobs, businesses are affected and our life as a nation is affected," amesema Ruto

Kiongozi huyu vile vile amesifia pakubwa hatua ya wakenya kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali na kuongezea kuwa wananchi wana imani serikali itaafikia kuweka mikakati mwafaka ya kufungua uchumi wa taifa.

"When you called the nation to action the response from Kenyans was unprecedented. Every Kenyan stepped forward,""As you mobilise the government to this guidelines,. We are confident that under your leadership the government will take necessary decision to ensure that we mitigate the effects of this pandemic," amesimulia Ruto

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kwa upande wake aliwatakia kila heri wakenya wanapoendelea kuadhimisha maadhimisho ya Madaraka japo wakiwa nyumbani kutokana na hofu ya corona.