Wakfu wa Victor Wanyama wasaidia familia za wakazi wa Korogocho

Wakfu wa nahodha wa timu ya taifa ya Harambee Stars, Victor Wanyama umeweza kusaidia familia ambazo zinaishi katika mtaa wa Korokocho.

Kupitia mtandao wake wa kijammi, Wanyama  alionesha jinsi wakenya wanaisghi katika hali duni katika mtaa huo.

Kupitia wakfu wake, Wanyama ambaye anachezea timu ya Montreal Impact, alijitolea na wakfu wake kuwajengea wenyeji wa Korocho nyumba za kisasa. Wanyama amewaomba wahisani kujitolea kuwasaidia wananchi hao ili wawe na maisha mema kuliko ya sasa.

Wanyama aliandika,

Corona imebadilisha maisha ya watu wengi kwa njia nyingi. Katika mtaa wa Korogocho familia nyingi zimewachwa bila makao bila mahala pa kulaza vichwa vyao. Wakfu wa Wanyama unawaomba kushikana nasi mikono katika harakati ya kupea familia hizi mahala pema.

(Totonto Korogosho Project.The Covid19 pandemic has changed people’s lives in very many ways. In Korogocho,families have been left homeless with nowhere to lay their heads on.The is appealing to each one of us to join hands in providing these families with a safe haven.)

Tazama video ifuatayo,