Wakimbizi wa Migori wataka kufidiwa

 Wakimbizi wa ndani kwa ndani kutoka kaunti ya Migori wameitaka serikali kuu kuwalipa fidia yao ya shilingi elfu mia mbili  kwa hasara waliopata baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.

Wakimbizi hao wanadai kuwa kuna njama ya kutoa majina yao kutoka  orodha ya wakimbizi iliyowasilishwa katika afisi kuu ya wakimbizi. Wamelalamikia hatua ya kucheleweshwa kwa fidia hiyo kwani baadhi ya wakimbizi kutoka sehemu nyingine za taifa walilipwa.