Walevi wa Bungoma washinikiza serikali ihalalishe busaa

Walevi wanaobugia pombe aina ya busaa kaunti ya bungoma sasa wanaishinikiza serikali ihalalishe pombe hiyo wakisema haina madhara ya kuharibu viungo vya mwili kama chang'aa.

Mzee patrick musiama mwenye umri wa miaka hamsini na saba anasema busaa inaongeza damu mwilini na haina madhara hivyo polisi hawafai kuwakamata watumiaji wa pombe hiyo. Isitoshe walisema kuwa pia inamfanya mtu aishi muda mrefu.

Haya ni kwa mujibu wa mzee Robert Khwenya ambaye pia hubugia busaa akisema ni pombe ya kienyeji na hutumika sana sana kwa sherehe za kitadamuni za jamii mbalimbali nchini.

La kushangaza ni kuwa awali pombe aina ya changaa iliitwa 'shauri yako' kwani ni wakati huo wa uongozi wa rais wa kwanza nchini hayati Jomo Kenyata ambapo vilabu vya busaa viliruhusiwa na vilichangia ukuaji wa uchumi kutokana na ukusanyaji ushuru.

Walevi hawa pia wanadai kuwa ndoa nyingi zinasambaratika kutokana na kuharamishwa kwa matumizi ya busaa kwani kulikuwa na utaratibu wa kudumisha maadili katika jamii.