Walimu katika shule za kibinafsi hawajalipwa kwa miezi mitatu

Walimu wengi katika shule za kibinafsi nchini hawajalipwa kwa miezi mitatu sasa kutokana na kufungwa kwa shule zote nchini kutoka mwezi Machi kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Soma pia;

Walimu wengi katika shule za kibinafsi hutegenea karo zinazolipwa na wanafunzi kupata mishahara yao. Wengi wao sasa wamelazimika kuanza kazi za vibarua na kazi zingine ndogo ndogo ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Serikali iliagiza kufungwa kwa shule zote  zikiwa zimesalia wiki tatu shule zifungwe kwa muhula wa kwanza. Siku ya Jumatano walimu wengi waliozungumza nasi walisema kwamba hawajalipwa mishahara ya miezi ya Machi, Aprili na Mei.

“Watu wengi hudhania kwamba walimu katika shule za kibinafsi hulipwa mshahara wa kuvutia lakini sio shule zote za kibinafsi zinalipa mshahara mzuri," mwalimu mmoja alisema.

Aliongeza kuwa "Walimu husubiri wazazi kulipa karo ndiposa walipwe na wazazi wasipoliwa basi wao pia hawalipwi."

Soma pia;

Mwalimu huyo anataka walimu katika shule za kibinafsi pia kuwekwa katika kundi la watu walioathirika sana na janga la virusi vya corona. Walimu katika shule za umma wanaendelea kulipwa mishahara bila tatizo lolote kwa sababu mishahara yao inalipwa na serikali kutokana na pesa za watoa ushuru.

"Serikali ilitenga mabilioni ya pesa ili kuwakinga wanamuziki, wanaspoti, wahudumu katika sekta ya utalii na vijana na kusahau sekta ya elimu," Msomi Hemed Mukui alisema.

Alitoa wito kwa serikali kuwasaidia walimu wote waliosajiliwa na tume ya TSC na ambao hawajaajiriwa na serikali.

Soma pia;

Duncan Ndiema Ndiwah afisa aliyeangamiza Yassin Moyo kutiwa mbaroni

Wengi wa walimu hao sasa hawawezi kumudu mahitaji yao ya kulipa kodi na mahitaji mengine ya kimsingi. Hali ni hiyo pia inawakabili wahadhiri katika baadhi ya vyuo vya kibinafsi huku wengi wao wakikatwa mishahara.