Wanamuziki wa kike wanaozengua wenzao wa kiume

Licha ya wanamziki tofauti kujitokeza nchini na talanta zao ,kunao wengine wa kike ambao wanawakosesha wenzao wa kiume lepe la usingizi kutokana na maumbile na urembo walio nao.

Katika muziki wa kale ni wengi waliowazengeun wenzao wa kuime kutokana na urembo wao ni kama Lady Jay Dee,Saida Karoli na katika kisasi kipya na cha kisasa waimbaji kama vile Avril,Akothee,Victoria Kimani wanawakosesha waume usingizi.

Wengi wa Wanamuziki hawa wanaimba nyimbo za Bongo  wakitokea taifa jirani la Tanzania na baadhi yao ni kama ifwatavyo.

1.Nandy

Anajulikana sana kwa nyimbo zake ambazo ametoa na kwa sauti nyororo inayofanya waume wengi kushika tama.

Nandy alienea sana alipotoa wimbo wake wa HALLELUJA NA NJIWA  akimshirikisha mwanamziki kutoka kenya Willy Paul.

'Hallelujah na Njiwa'.

3.Vanessa Mdee

Ni malkia wa nyimbo xza kisasa akitokea taifa jirani la Tanzania na alianza kutawala mawimbi ya mziki alipotoa wimbo wake wa kwanza na mwanamziki mwemnzake Ommy Dimpoz kwa jina ME and YOU.

Kama vile Ruby Vanessa amekaa katika sanaa ya muziki.

4.Rosa Ree

Mmmh sema mrembo kupindukia, Rosa alitambaa mitandaoni baada wa wimbo wake akimshirikisha mwimbaji tokea kenya Timmy T Dat.

Lakini si urembo tu pekee bali mtirirko wa nyimbo zake zinaweza tu kuimbwa na si mwingine bali ni Khaligraph.

5.Queen Darleen

Wengi wanamfahamu kama dada  mwimbaji wa nyimbo za kisasa  Diamond lakini talanta yake haiwezi fungiwa wala kukataliwa katika sanaa yake.

Aliutoa wimbo wake akimshirikisha Ravanny'kijuso' uliogonga  katika uganda wa afrika mashariki na hata magharibi kwa kipindi kirefu.

6.Aika (Navy Kenzo)

Aika ni mpenzi wake Narheel na wawili hao walijulikana sana baada ya kutoa wimbo wao wa kwanza  'Kamatia'