wanamuziki (1)

Wanamziki wa nyimbo za injili wanaopendeza zaidi Kenya

Kutokana na utafiti wa Radio Jambo, tuliweza kuandaa orodha ya wanamziki wa injili ambao kulingana na sisi, tunaona ni wanamziki ambao wameumbwa wakaumbika, yaani vidosho, aisee, vitoto 10/10, maanake kumi juu ya kumi.

  1. Kambua Manundu

Kambua Manundu ni mtoto wa pili kwa familia ya watoto watatu wa hayati, Professor Manundu na Bi Lois Manundu. Kidosho huyu amezaliwa na kulelewa Mjini Nairobi. Zaidi ya hayo, binti Manundu alifunga ndoa za maisha na mpenzi wake, Bwana Jackson Mathu ambaye ni mfanyi biashara.

Hivi Majuzi, bwana na bi Mathu waliweza kupokea zawadi bora zaidi, zawadi ya mtoto wao Nathaniel Mathu.

Tazama Picha Zifuatazo za Mrembo Kambua.

Kambua-Covercover2cover 3

2. Emmy Kosgei

Emmy Kosgei ni mmoja wa wanamziki wa mumu humu Kenya, waliobarikiwa sana, si kwa sauti, sura, tabasamu na talanta ya utunzi wa nyimbo.

Mrembo huyu alifunga pingu za maisha na mpenziwe Bishop Anselm Madubuko, mwezi wa nane, mwaka wa elfu mbili kumi na tatu.

Ama kwa hakika, mapenzi ni bahari yasiyo na mwisho, kwani Mrembo huyu Emi, anaendelea kulisukuma gurudumu la mapenzi na mpenzi wake Bishop Anselm.

Tazama picha za mrembo Emmy Kosgei.

download emmydownload emmy 2

emmy hubby

3. Esther Wahome.

Mwanamziki huyu, aliyeitikisa mji na wimbo wake ”kuna dawa”, ni binti ambaye uzuri wake unaonekana mpaka wa sasa kwani pia naye, Jalali alimuumba kwa udongo mzuri. Licha ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili, Esther ameolewa na mpenzi wake, Bwana Godfrey Mureithi na pamoja, wana watoto watatu, Michelle Mumbi, Eldad Mureithi na Medad.

Je? uzuri upo ama haupo?

wahomewahomee2wahome 3

4.Mercy Masika

Mercy Masika, binti mwenye uweusi uliokolea vizuri, ni mwanamke ambaye, mziki wake umekuwa ukiwabariki wengi na bali na kuwa na sauti nzuri,urembo wake pia unawavutia wengi.

 

masikamasika 2masika 3

 

5.Gloria Muliro

Gloria Muliro aliyejulikana kwa wimbo wake na Willy Paul, ”sitolia” ni kipusa ambaye uzuri wake unaonekana kwa sura yake nzuri na pia kwa ukarimu wake wa kusaidia watoto kupitia kwa nyumba yake ya watoto, Gloria Children’s Home.

muliro 1muliro 2muliro 3

 

Iwapo una orodha ya wanamziki wa nyimbo za injili ambao kwako ni vidosho, usisite kuandika kwenye sanduku la maoni kwani waingireza walitusisitizia kuwa ”beauty lies in the hands of the beholder.”

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments