Wanandoa waita watoto wao corona na covid baada ya kujifungua mapacha

small-tiny-twins-newborn-african-260nw-671128750
small-tiny-twins-newborn-african-260nw-671128750
Virusi vya corona vimethibitishwa nchi tofauti huku vikisababisha vifo vya watu zaidi ya 51,000 lakini janga hili halikuwazuia wanandoa wa nchi ya India kuwaita watoto wao corona na covid.

Walisema kuwa waliwaita mapacha wao hivyo ili kukumbuka maishani shida ambazo alipitia mkewe alipokuwa anaenda kujifungua kwa sababu hakukuwa na magari na tayari kulikuwa na amri ya kutotoka nje.

Licha ya changamoto hizo, mkewe alijifungua vyema na wako na afya njema akiwa na mapacha wake.

"I was blessed with the twins - a boy and a girl - in the early hours on March 27. We have named them Covid (boy) and Corona (girl) for now. I had some difficulties before delivering the babies." Verma, 27 Alizungumza.

Kulingana na Verma, virusi vya corona ni hatari kwa maisha ya wanadamu na imewakumbusha wanadamu kuwa wasafi.

"The virus is dangerous and life-threatening but its outbreak made people focus on sanitation, hygiene and inculcate other good habits. Thus, we thought about these names." Alieleza Verma.

Alifichua na kusema wafanya kazi wa hospitali waliwaunga mikono kwa kuwaita mapacha hao majina ya virusi hivyo.

Verma alisema kuwa wanafamilia yao hawakuamini kuwa anaweza kujifungua kwa maana hakukuwa na magari ambayo yalikuwa yanasafiri wakati huo.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo alisema majina ya mapacha hao yamefanya hospitali hiyo kuvutia wengi.