Wanawe Felicien Kabuga wanataka mahakama ya Ufaransa kumwachilia

kabuga-children
kabuga-children
Wanawe Felicien Kabuga ,mshukiwa mkuu wa mauwaji ya halaiki ya watu katika taifa la Rwanda mwaka 1994 wameitaka mahakama kuu ya Ufaransa kuachilia janadamu hilo wakisema wanakiuka haki zake za kimsingi kwa  kuendelea kumzuilia mahakamani.

Kabuga wa 87 alitajwa na UN kama mshukiwa mkuu aliyeongoza maangamizi ya jamii ya Tutsi na kuchochea vita vya kijamii katika taifa hilo  la Afrika kisha kutorokea Ufaransa.

Amekuwa akizuiliwa katika mji mkuu wa Paris tangu Mei 16 alipotiwa mbaroni ikihitimisha miaka 26 ambayo alikuwa mafichoni na akitafutwa .

Mahakama za Ufaransa zitaamua iwapo watampelekea katika mahakama za Jumuiya ya Kimataifa UN Juni 3.

Wanawe sasa wanataka mahakama hizo kumwachilia kutokana na hali yake ya afya kuwa mbaya.

“In recent years he has accumulated many pathologies: diabetes, hypertension and severe senile dementia,” .“He also had a colectomy last year. His state of health requires support and constant surveillance, like any weak and dependent elderly person,” the statement said, adding that he had lost weight and become more incoherent since his detention.taarifa kutoka kwa wanawe 11