‘Wangu peke yangu,’ Dada yake Diamond Darleen amwambia mke wa kwanza

Dada yake msanii wa bongo Diamond Platnumz Queen Darleen alimwandikia mumewe Isihaka Mtoro ujumbe wa mapenzi kwenye mitandao ya kijamii. Queen aliolewa na Mtoro mwaka jana Desemba kama mke wa pili.

Akiwa kwenye mahojiano, Darleen alisema kuwa alijua mumewe ana mke wa kwanza na hawajawahi kupatana bali huwa wanazungumza tu.

Kupitia kwenye mitandao Darleen alisema kuwa Mtoro ni wake peke yake na hamna mtu mwingine,

"NI WACHACHE SANA WENYE MAPENZI YA KWELI WENGI WAO NI WASANII WA MAIGIZO YA MOVIE YA MAPENZI INA MAANA ATA MOVIE IWE NDEFU VIPI LAZIMA ITAKWISHA TU NA INA AINA MBILI ZA UISHAJI WAKE EIZA UWE MWISHO MZURI AU MBAYA IWE IMEKUSIKITISHA AU IMEKUFURAHUSHA IYO NDIO HALI ILIYO SASA KWENYE MAISHA YA MAPENZI I LOVE YOU ISIHAKA MTORO WANGU @ISIHACK WA KWANGU MIMI PEKEANGU ❤🙏❤ #PARKINGYAISIHAKAMTORO." Aliandika Queen Darleen.

Dada yake Queen Esma Khan kwenye sekta ya maoni alimuuliza kama alikuwa amemsahau bibi wa pili na alikuwa na haya ya kumjibu,

‘WEEE CHAKUFIA HIII NYIE HUYU PEKE YAKO HIYO KWIOOOO KWA HIYO UNAMDELETE MWENZIO EEEEH!!!’

Uvumi unao habari kuwa Queen Darleen ni mjamzito, ilhali alikuwa na mtoto kabla ya kuolewa na Mtoro.