Wanne wafariki baada ya kupigwa risasi, polisi wasimulia kisa

Washukiwa wanne wa ujambazi wamepigwa risasi na polisi  katika eneo la Juja baada ya jaribio lao la wizi.

Majambazi hao walikuwa miongoni mwa genge la watu 6 ambao wamekuwa wakiwaibia watu katika barabara kuu ya Thika.

Wanne hao walikumbana na mauti yao baada ya kukabiliana na maafisa wa polisi mwendo wa saa 4 alfajiri Jumapili.

Soma hadithi nyingine:

Kamanda wa polisi katika kanda ya Nairobi Philip Ndolo alisema kwamba washukiwa hao walikuwa wamewaibia baadhi ya wakaazi na walikumbana na mauti yao walipokuwa wakitoroka.

"Washukiwa hao wanne wamekuwa wakiwahangaisha wakaazi kwa wizi hususan waendeshaji boda boda. Polisi hawakuwa na jingine walipoarifiwa na umma. Makabiliano kati ya polisi na majambazi yaliishia kuwa mauti kwao, " Ndolo alisema.

Alisema kwamba genge hilo ni miongoni mwa lile linalowaibia wakaazi pesa, simu na mali nyingine. Pia wanashukiwa kwa utekaji nyara na wizi wa magari ambao umekithiri huku Nairobi.

Ndolo alisema kwamba polisi walipata bunduki mbili pamoja na risasi kadhaa na visu 4 kutoka majambazi hao.

"Tulipopata ripoti kutoka waathiriwa, wajasusi kutoka kituo cha polisi cha Pangani walianza kuwasaka. Polisi  walipowapata 6 kati yao, walikaidi amri ya kujilazimisha na ufyatukaniaji wa riasi ukaanza" Ndolo alisema.

Polisi wanasema kwamba wawili walitorokea katika mtaa wa Kosovo huku wakiwa na majeraha ya risasi.  Mili ya waliouliwa ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hosipitali kuu ya Kenyatta.

Mkaazi aliyepigwa kichwani na majambazi hao, aliripoti kwamba alikuwa langoni akisubiri ufunguliwe alipovamiwa na kuamrishwa kupeana mali yake  yenye dhamani.

Kulingani na polisi, washukiwa hao waliuliwa siku moja tu baada ya aifsa mmoja wa polisi kuvamiwa katika mtaa huo.