unnamed (20)

Wanted! Maafisa wa polisi waanzisha msako wa jamaa wawili waliomuua mwanahabari

Maafisa wa ujasusi kutoka kitengo cha DCI nchini wameanzisha msako mkali dhidi ya washukiwa wawili wakuu wanaoshukiwa kuhusika katika mauaji ya mwanahabari wa redio ya Pamoja Fi Mohammed Marijan.

Wawili hao Brian Kenani almaarufu kama Kaisilo na Fazul ni miongoni mwa watu sita ambao walinakiliwa na kamera za siri wakimshambulia mwendazake.

Jamaa wa miaka 72 atiwa mbaroni kwa kumnajisi msichana wa miaka 17-Homa Bay

“Any person with any information that may lead to the arrest is requested to report to DCI Kilimani or at the nearest police station,” “The information will be treated with a lot of confidentiality,”DCI imesema

Brian Kenani alias Kaisilo, alias Fazul (above) is wanted by DCI.

Vimbwanga hivi! Amos Kimunya aondolewa kesi ya wizi wa milioni 60

Mauaji ya mwanahabari huyo yalifanyika mnamo Mei 4 katika mitaa ya mabanda ya Kibra mida ya saa 4 asubuhi alipokuwa anatoka kazini.

 

Mei 11, mshukiwa mmoja kwa jina Juma Hussein Muhammed alotiwa mbaroni kuhusiana na kisa hicho na kuzuiliwa kwa siku tisa zaidi.

Wakaazi wa mtaa huo wa Kibra sasa wanasema kuwa mahakama za eneo hilo zimekuwa zikitumika kuwaficha washukiwa hatua ambayo wameitaka serikali kuingilia kati.

 

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments