Washukiwa watano wakamatwa kwa kujaribu kumhonga afisa wa polisi

Watu watano wamekamatwa na kilo 700 za bangi yenye thamani ya shiling 4, iliyopatikaa katika shamba moja eneo la Juja kaunti ya Kiambu. Mkuu wa DCI George Kinoti anasema washukiwa hao walijaribu kumhonga afisa mkuu wa polisi kwa shilingi laki sita alfu 89. Pesa hizo pamoja na bangi hiyo inazuiliwa ili kutumika kama ushahidi kortini.

Kwingineko, polisi huko Samburu wamewakamata watu wakumi wanaoshukiwa kuingia humu nchini kinyume cha sheria. Niabu wa mkuu wa polisi Abdikadir Malicha anasema washukiwa hao ambao ni raia wa Ethiopia walikamatwa katika bara bara ya Barsaloi na Maralal muda wa saa nane usiku. Washukiwa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Maralal.

Hayo yakijiri, kesi ya msichana mwenye umri wa miaka 15 aliyemuua  mpenzi wake, kijana mwenye umri wa miaka 19 katika mtaa wa Langa'ta siku ya jumatano wiki jana itasikizwa kesho. Hakimu wa Kibera Esther Boke amemshauriwa afisa wa uchunguzi kuhakikisha wanasalimisha mahakamani ripoti ya uchunguzi wa kiakili na udhibitisho wa umri ili kuamua iwapo yuko sawa kuhukumiwa, huku ripoti ya uchunguzi wa mwili wa mwendazake ukisubiriwa.

Msichana huyo anashukiwa kumdunga kisu mara tatu kifuani aliyekuwa mpenzi wake kufuatia ugomvi.