Wataka Kuoa? Mke Ni Gharama. Jipange

Vijana wengi walio katika umri wa kuoa siku hizi watakwambia bado wanasubiri kwanza kwa sababu wanawake wamekua na mahitaji mengi.

Hata hivyo mtaalam wa maswala ya uhusiano Chris Hart anasema swala ku sio ati wanawake wamekua na mahitaji mengi bali ni wanaume kukosa kutokua na uwezo wa kuyakidhi haya mahitaji ya wanawake.

Kutokana na kisingizio hiki, utakuta wengine wanaamua kuoa wanawake wazee .

Mtaalam Cheis Hart anasema mara nyingi vijana wanaamua kuoa wanawake wazee sababu kuu hua sio mapenzi.

Anasema hua wanalenga tu kuwanyonyoa hela na mali zao. Anasema ni vijana wachache sana wanaoa wanawake wazee kwa sababu ya mapenzi.