Watano wafariki, Je ni nini kilichosababisha ajali hii?

ajali
ajali
Watu watano wamefariki baada ya ajali kufanyika kwenye barabara ya Nairobi-Kangundo mtaa wa kamulu.

Polisi wa kaunti ndogo ya kayole bwana Wilson Kosgei alisema kuwa ajali hii ilikuwa kati ya gari la kibinafsi na basi la kampuni ya Kenya Bus Services.

Mashahidi walizungumza na gazeti la Star na kusema kuwa, ajali hii ilitokea baada ya dereva aliyekuwa akiendesha gari akielekea Nairobi alijaribu kupiku gari aina la salon kisha ghafla basi hilo likagongana na gari jingine ana kwa ana.

Kosgei alisema kuwa, watu watano walifariki papo hapo .

Zaidi ya hayo, watu wengine 17 walijeruhiwa sana na  kukimbizwa kwenye hospitali ya Mama Lucy ili kupata matibabu.

Miili ya waliofariki ilipelekwa kwenye mochari ya City.

Vilevile, Kosgei alisema kuwa polisi wameanza kufanya uchunguzi zaidi ili wajue ni nini hasaa kilisababisha ajali ile.

Kosgei aliwatahadharisha madereva kuhusu uendeshaji wa ovyo wa magari  na kusema kuwa uendeshaji mbaya wa magari una malipo na malipo yake si matamu.