Watatu Wauliwa Kwa Kushukiwa Kuwa Wachawi Kilifi

Wanawake wawili na mwanamume mmoja wameuliwa kwa kudaiwa kuwa wachawi katika kaunti ya Kilifi.

Wakaazi wanadai kwamba watatu hao walimroga mhudumu wa boda boda aliyezama maji wikendi iliyopita.

Wananchi waliojawa na gadhabu wanasema kwa sasa wanawasaka wengine wanne wanaodaiwa kujihusisha na uchawi.

Visa hivi vimekua vikiendelea sana katika kaunti ya Kilifi huku wazee wenye mji wakishukiwa kuwa wachawi. Wengi wao wametafuta hifadhi katika kaya Godhoma wakihofia kuuliwa.