Wasanii wa kenya ambao watoto wao wana majina ya kipekee

Wasanii wengi huwa katika mstari wa kwanza katika habari waendapo kubarikiwa na watoto, lakini si wote ambao wana majina ya kipekee baadhi ya watoto hao ni kama vile wafuatao;

Pierra Makena

Ni DJ ambaye anafahamika sana na usanii wake ,alibarikiwa mtoto wake wa kwanza msichana mwaka 2016 na kumpa jina Ricca Pokot.

Bahati na Diana Marua

Hawezi saulika katika kitengo hicho cha kuwapa majina watoto huku kitinda mimba wakimuita Majesty Bahati na msichana wao wa kwanza akiitwa Heaven Bahati.

Size 8 na DJ Mo

Walijaliwa na kifungua mimba ambapo walimuita Ladasha Belle jina ambalo si rahisi kupata na  lina maanisha zawadi nzuri kutoka kwa mungu.

Nick Mutuma

hajaoana na baby mama wake bali walikaa chini na kuonyesha mtoto wao upendo jina ambalo linamaani Maombi.

Pitson

Mwanamziki huyo wa nyimbo za injili alibarikiwa na mtoto msichana ambaye jina lake lina maanisha pahali pa dhahabu jina hilo ni Havila.

Bridget Achieng

Alibarikiwa na mtoto wa kiume na kumuita jina Sekani Rich

Janet Mbugua

Mwana habari huyu amebarikiwa na vijana wawili waliofahamika kama Huru Ndichu na Mali Ndichu

Mr Seed

Msanii Seed alibarikiwa na mtoto kijana mwaka jana na kisha kumuita Gold Christen.

Nameless na Wahu

Wana msichana ambaye urembo wake ni wakupigiwa mfano si urembo tu bali jina lake ni la kipekee Tumiso ambalo lina maanisha msifuni Mola.