Watu 13 waangamia katika ajali ya barabarani Awasi

AJALI
AJALI
Watu 13 wameaga dunia , katika ajali mbaya ya barabarani huku wengine wengi wakijeruhiwa katika eneo la Awasi kwenye barabara kuu ya Kisumu Kericho.

Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya saa sita usiku na ilihusisha basi la kampuni ya Eldoret Express na trela na zilizogongana ana kwa ana.

Polisi wamethibitisha ajali hiyo na kusema kwamba wahasiriwa 35 wakiwa na majeraha kadha wa kadha wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga, Awasi Mission Hospital na Hope Medical Hospital.