Watu 175 wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu dhidi ya corona

EaJuvVRWAAAMEeC.jfif
EaJuvVRWAAAMEeC.jfif
Katibu msimamizi katika wizara ya afya nchini Rashid Aman amesema kwa mara nyingine tena serikali imewaruhusu watu 175 kutoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha watu 1048.

Wakati uio huo watu wengine 105 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo na kufikisha watu 3094.

Kati ya visa hivyo vipya vya maambukizi ,wakenya ni 96 huku raia wa kigeni wakiwa 9.

Visa vilivyosajiliwa katika kaunti ya Kisumu na Busia vimetokana na madereva wa malori waliofanyiwa vipimo.

Aidha mtu mmoja amepoteza maisha yake kutoka na virusi hivyo na kufikisha watu 89 waliofariki.

Aman amesema kutokana na ongezeko la madereva wa masafa marefu kuendelea kuandikisha idadi  kubwa,serikali imeanza kuweka mikakati ya kusaidia kaunti hiyo ili kuzuiya maambukizi.

Nairobi imeandikisha visa 43 huku kaunti ya Busia ikiandikisha 18.

Aman pia amezindua mradi wa kuanza kuwahudumia wagonjwa wa corona nyumbani ambao hali yao ya afya si mbaya ikilinganishwa na baadhi ya wagonjwa wengine.

Kufikia sasa Kenya imwapima watu 102,956 kuhusiana na virusi vya corona.

Katika takwimu za hii leo wanaume ni 77 huku wanawake wakiwa 28.

Waathiriwa ni wa umri wa kati ya miaka miwili  na 77.

Visa hivyo vimetokea maeneo yafuatayo Nairobi, 43 Busia, 18 Mombasa, 11 Turkana, 7 Migori, 6 Kwale & Kiambu, 5 cases each, Kilifi, Machakos na Taita Taveta 3 , Kisumu, 2 Uasin Gishu, Siaya, Kajiado na  Garissa, ikisajili kisa kimoja.