Watu 254 wamepatikana na virusi vya corona- Mwangangi

Dr-Mercy
Dr-Mercy
Katibu msaidizi katika wizara ya afya nchini Mercy Mwangangi amesema kuwa watu 254 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli za watu 4, 859 kufanyiwa vipimo na kufikisha wagonjwa 5,206 walioambukizwa virusi hivyo.

Wakati uo huo watu 41 wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupona na kufikisha takriban watu 1823 waliopona.

Aidha taifa limepoteza watu wawili kutokana na ugonjwa huo na kufikisha watu 130 walioangamia kutokana na corona.

Kufikia sasa Kenya imewapima watu 151,396 kuhusiana na corona.

Waathiriwa hao wote ni wakenya huku wanaume wakiwa 186 ,wanawake wakiwa 68.

Waathiriwa ni kati ya miaka 4 hadi 92.

Nairobi kati ya visa hivyo imesajili watu 127,Mombasa 36,Migori 29,na kaunti ya Kajiado ikasajili visa 22,Kiambu12,Uasin Gishu 5,Murang'a 3,Machakos ,Kilifi zote visa 2,Nakuru,Siaya,Taita Taveta,Kakamega na Kisii zimesajili kisa 1.