Watu 40 watiwa mbaroni kwa kukosa kuzingatia amri ya serikali kaunti ya Kisumu

Japo taifa la Kenya limekuwa likiwahimiza wananchi wake kuheshimu maagizo yanayotolewa na maafisa wa afya ili kupunguza maambukiz ya virusi hatari vya corona nchini, jamaa 40 katika kaunti ya Kisumu wametiwa mbaroni baada ya kupatikana wakifanya mazoezi ya kukimbia kwa ukaribu sana bila ya kuzingatia umbali wa mita moja unusu.

Yakijiri hayo, mbunge wa zamani wa Kasarani John Chege amepatikana na makosa ya kuitisha shilingi elfu 100,000 kutoka kwa mwanakandarasi ili kulipa shilingi milioni 3.3.

Ameachiliwa kwa dhamana ya milioni 1.3.

Yanajiri haya huku polisi katika mitaa ya Kayole wakiwanasa jamaa watano waliokuwa wanakunya pombe licha ya serikali kupiga marufuku watu kutangamana eneo moja.