Watu 72 wameruhusiwa kuondoka hospitalini- Rashid Aman

Katibu msimamizi katika wizara ya afya Dr Rashid Aman amesema watu 72 waliokuwa wamelazwa hospitalini baada ya kuambukizwa virusi vya corona sasa wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupata nafuu.

Kufikia sasa, Kenya imeandikisha watu 1164 waliopona kutokanana virusi hivyo.

Wakati uo huo watu 90 wamepatikana na virusi hivyo na kufikisha watu 3305 walioambukizwa.

Watu 62 ni wanaume huku wanawake wakiwa 28.

Kaunti ya Nairobi iko na visa 36 huku Mombasa ikiwa na 34.

Visa 12 vilivyoandikishwa katika kaunti ya Busia ni madereva wa Malori waliotokea katika mpaka wa Malaba.

Watu wanne wanaripotiwa kuaga dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha watu 96 waliofariki.

Aman wakati uo huo amezindua mpango wa wananchi kujitokeza na kutoa damu ili kusaidia kuongeza idadi ya damu katika hosptali mbalimbali nchini.

Kufikia sasa Kenya imewapima watu 108,666 kuhusiana na virusi hivyo.