Waziri Karanja Kibicho aeleza kuhusu kadi ya kisasa ya huduma

the_national_integrated_identification_management_system_niims_kenyans_are_against_huduma_namba
the_national_integrated_identification_management_system_niims_kenyans_are_against_huduma_namba
Waziri wa mambo ya ndani Karanja Kibicho aliweza kusema kuwa gharama ya mradi wa namba ya kisasa ya huduma ina sehemu tatu kwanza ikiwa ni kununua mashine elfu thelathini na moja mashine ambazo zimechukua gharama ya billioni 1.7 mradi ambao ulikamilika.

Pili aliweza kuzungumzia kuhusu wafanyakazi 50,000 ambao watakao wasajili wananchi, alisema kuwa watakuwa wakilipwa shillingi 1500 kwa siku moja.

"Tumechukua watu watano katika kila kata ndogo, si wananchi wa kutoka nje ilhali ni wa kenya tu watakao sajili wananchi wenzao huku wakifanya kazi wa siki tisini," Alieleza kibicho.

Alisema kuwa hiyo ndio ilikuwa gharama ingine kubwa waliokumbana nayo kama wizara, gharama ya tatu alisema kuwa ilikuwa ya kununua sombezo za programu yaani (software).

"Tuliweza kusikizana kama wizara tuweze kuchukua vijana wa nchi yetu waweze kutengeneza Sombezo hizo,

"Hii ni kwa sababu tuliona kufanyiwa sombezo hizo nje ya nchi itachukua muda na pia gharama itakuwa juu zaidi, kwa hivyo tulichukua vijana ambao wamesomea kazi hiyo na kutengeneza," Kibicho aliongea.

Aliongeza na kusema kuwa ili kukuja na sombezo hilo waliweza kutumia billioni tano hadi sita, huku akisema kuwa katika maisha ya wakenya hawataweza kutumia pesa hizo tena kama vile zilizo tumika katika mradi huo.

"Hizo pesa tutaweza kuziregesha kwa muda wa miaka kumi huku tukiwa tumepata manufaa mengi kama wananchi, itaweza kusaidia pia kusajili wakati wa kipiga kura katika maisha ya usoni," Alizungumza Kibicho.

Kibicho alisema kuwa watoto wataweza kusajiliwa wakifika miaka sita kwa maana watakuwa wamefikisha umri wa kuenda shule, pia mtoto aaweza kupewa namba ya masomo ya Nemis  shuleni kisha apewe namba ya huduma.

Alizungumza na kusema kuwa wataunganisha namba hiyo na Nemis na huduma iliziweze kufanya kazi moja, aliongezea na kusema kuwa watoto ambao watakao zaliwa badala ya kupewa cheti cha kuzaliwa wataweza kupewa namba hiyo ya huduma.

Katika kila kituo kutakua na machine tano na maafisa wa kusajili watano, alisema pia mwananchi ataweza kujisajili mahali popote alipo na si mashambani.

"Si kweli kuwa tutaweza kuchukua chembechembe za damu za wananchi, tutafanya tu kupiga wananchi picha pekee, sisi kama wizara na serikali hatuna haja ya kuchukua chembechembe za damu (DNA),

"Kama mwananchi ukibadilisha jina mashine hiyo itaweza kujua, ata waliofanyiwa majaribio hawakutolewa damu, pia itaweza toa maelezo ya mashambani," KIbicho aliongea.

Alisimulia na kusema kuwa mashine hizo zina manufaa tofauti kama vile kujua wananchi ni wangapi pia kama kuna  mradi wowote wataweza kujua ni wananchi wagani watatumia mradi huo na kadhalika.