'Weka ya baby mama.' Rayvanny aambiwa baada ya kuchora tattoo yake ya kwanza

Msanii wa nyimbo za bongo Rayvanny kwa mara ya kwanza amechora tatoo katika shingo lake kama wale wasanii wengine huanza na kuchora mikono.

Yake iliwavutia wengi hasa wasanii wenzake, ambayo alichora ikisoma 'blessed' yaaani kubarikiwa.

Kupitia mtandao wa kijamii, aliposti picha na kuandika maelezo mafupi.

"BLESSED. NGOZI TAA IMEWAKA ." Aliandika Rayvanny.

Wasanii wenzake Diamond Platnumz na Mbosso walionyesha upendo wao kwake kwa kunakili na Emoji za upendo huku nduguye Diamond, DJ wa WCB na Rommy Jones wakimshawishi afuate nyayo za Diamond.

"HAPO BADO JINA LA MTOTO, MAMA NA MAUA YAAANZE RASMI." Aliandika.

Kwa mkono wake wa kushoto, Diamond amejaza majina katika tatto zake huku jina la kwanza likiwa la baby mama wake Zari Hassan.

Tatto ingine ya majina ya watoto wake wakiwa na Zari.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO