Wezi wavamia mkahawa na kuitisha mvinyo kabla ya kuanza kuiba

ROBBERY
ROBBERY
NA NICKSON TOSI

Meneja wa mkahawa wa kuuza mvinyo Afrika Kusini ameelezea stesheni ya eNCA kuwa genge la wezi lilivamia mkahawa wake usiku na kuagiza mvinyo kwanza kabla ya kushurutisha kuwaonyesha eneo analoweka bidhaa muhimu kwa mkahawa huo.

“Mwanza waliagiza vinywaji kwanza  na hatimaye wakaniamrisha niwaonyesha sehemu moja ya mkahawa huo wangu ninakoweka vitu vyangu muhimu." Ameeleza Willie Kruger.

Japo taifa hilo la Kusini mwa Afrika limesitisha baadhi ya masharti yake, uuzaji wa vileo ungali haujaruhusiwa.

Kamera za siri zilizoonyeshwa na Televisheni ya eNCA, zilionyesha wezi hao wakiburura friji iliyokuwa imejaa vinywaji wakiondoka navyo.

Kitendo hicho kilitokea masaa machache tu kabla ya mida ya watu kuwa ndani ya nyumba zao kufika.