Wikendi Tutakuwa Paris Kwa Sherehe Za Mwanawe GIDI- Ghost Mulee (VIDEO/PICHA)

Siku ya Ijumaa mtangazaji maarufu, Ghost Mulee alifichua kuwa atakuwa Ufaransa katika mji mkuu wa Paris, ambapo pamoja na mwenzake Joseph Ogidi watasherehekea siku ya kuzaliwa ya Marie-rose Hera Ogidi, mwanawe Gidi.

Mpenziwe Gidi na mwanawe wanaishi mjini, Paris, Ufaransa.

Marie-rose Ogidi ambaye alizaliwa tarehe ishirini na mbili mwezi Mei mwaka wa 2016 atasherehekea mwaka mmoja katika kipindi cha juma moja lijalo.

Hatua hii ya bwana Ghost kuungana na 'boss' wake iliwafurahisha wapenzi wa kipindi chao maarufu, kwani wengi walipendezwa na umoja na ushirikiano kati ya wawili hao ambao wamekuwa wakipeperusha kipindi hicho cha asubuhi pamoja kwa mda wa zaidi ya miaka minane sasa.

Gidi ambaye hajakuwa hewani tangia siku ya Alhamisi, aliondoka siku ya Jumatano usiku huku akitangazia waskilizaji wake kuwa lazima angesafiri kuungana na familia yake, huku akimtarajia bwana Mulee aungane naye.

Sherehe za mwanawe Gidi, zinaambatana na siku ya kuwasherehekea wanawake haswa kina mama wote dunia na Ghost alisikitika kuwa hatakuwa na mkewe mpendwa, lakini ana furaha mpwito mpwito kwani atakuwa akimsherehekea mama Marie-rose Ogidi nchini Ufaransa.

"Katika siku ya wamama nasikitika sitakuwa na mamangu mzazi kwani alifariki kitambo lakini mke wangu ni mama kwa hivyo namtakia siku ya kufana ya kina wamama. Wikendi hii lakini nasafiri hadi Paris maanake kuna sherehe za mtoto wa Gidi boss wangu. " Alisema Ghost.

Unajua boss wako usipoenda sherehe zake hapo ndipo uhondo hutokea mara ooh unajua Ghost amekuwa akikohoa kwa studio. Kwa hivyo lazima usimame na boss wako. Halafu itakuwa wikendi ambayo timu ya raga nchini itakuwa ikicheza kwa hivyo lazima tuhudhurie! Tuko ndaani ndaani ndaani ya Sevens. " Aliongeza bwana Ghost.

Pindi tu Ghost alipofika, Gidi hakuchelewa kupiga picha naye pamoja na familia yake huku wakijitayarisha kwa sherehe. Tazama picha zifuatazo.

Twawatakia watangazaji hawa wawili wikendi ya kukata na shoka.