Wilbroda: Sababu ya kuacha kipindi cha Papa shirandula

Kipindi ambacho kinawachekesha wengi na kuvutia wananchi wengi, wataweza kuigiza kipindi hicho bila Wilbroda almaarufu Jacquey Nyaminde ambaye alikuwa anaigiza kama bibi yake Papa shirandula.

Jacquey alisema kuwa hawajakuwa wakielewana kwa muda sasa na papa Shirandula kwa majina kamili Charles Bukeko.Kipindi ambacho kimemilikiwa na kampuni ya Royal Media Services.

"Ata hivyo sisi ni marafiki wa kufana na pia huwa tunaongea huku nje," Wilbroda alieleza.

Katika habari Charles Bukeko alimtoa Wilboda katika kipindi hicho baada ya kujiunga na radio ya milele ambayo iko ndani ya Mediamax.

"lakini mnapaswa kuwa na hakika kuwa mtaniona tena katika televisheni zenu nikifanya vipindi vingine ambavyo niko ndani."

"Kuna mambo mazuri ambayo yako mbele yangu,lakini kuna mambo ambayo yana paswa  kunyamaziwa lakini yakikuwa sawa nitaweza kujulisha dunia."

"Tuliweza kumfikia meneja wa kipindi hucho na kusema kuwa Wilbroda yupo katika kipindi cha papa Shirandula na kama amewacha kuigiza labda anajua vizuri zaidi lakini kwa sasa Wilbroda yuko katika kipindi hiki."