Willy Paul Apongezwa na wenzake kwa kumrai rais Kenyatta walipwe kama wasanii

NA NICKSON TOSI

Ni wiki moja ambapo msanii Willy Paula alimwandikia rais Kenyatta barua ya kumrai kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wasanii wa humu nchini wanalipwa haswa wakati huu ambao taifa la Kenya linakabiliana na vita dhidi ya Corona. Hatimaye, rais Uhuru Kenyatta alitangaza kuwa serikali yake imetenga takriban milioni 200 na milioni 100 kutoka kwa wizara ya michezo na zitamadu kama hela zitakazotumiwa kulipa wanamziki wa humu nchini.

Akisifia hatua ya rais Kenyatta, Willy Paul alikuwa na haya ya kusema .

Asante rais Kenyatta kwa kusoma barua yangu na kujibu maombi yetu kama wasani, lakini cha kusikitisha ni kuwa hela hizo zinapelekwa kwa afisi ambazo zinaongozwa na vibaraka ambao wamekuwa wakitulipa malipo duni. Aliandika Willy Paul.

Akimpongeza Wiliy paul, alikuwa msanii Frasha ambaye alisifia pakubwa hatua za msanii huyo kumwandikia rais Kenyatta barua, akisema ni sharti wasanii wa humu nchini wasimame wima na kupigania haki zao.

Asante kaka kwa kutuwakilisha vyema na pia ifahamike kuwa tunawakashifu wale watu wanaowanyanyasa wasanii wa humu nchini haswa katika shirika la kutetea maslahi ya wasanii MCSK . Aliandika Frasha .