Willy Paul atokea na skendo mpya. Ampiga na kutishia kumuua mwanadada

Staa na profesa wa muziki Afrika Mashariki Willy Paul amekumbwa na skendo mpya baada ya mwanadada aliyekuwa anadaiwa kutoka naye kimapenzi kufunguka A-Z kuhusu jinsi staa huyu alimfanyia ufedhuli na kumpiga kinyama. Susan Mwaniki amefunguka jinsi Willy Paul alimpiga na kumjeruhi.

Soma hapa:

Susan anahoji kuwa Willy Paul alimnyonga na baadaye kumtishia kumdunga kwa kisu. Aidha Susan anasema kuwa Willy pozze alichemsha maji ya sufuria kumchoma katika nyumba yake Syokimau.

Soma hapa:

 "Huwa hana mchezo akiamua kukifanya kitu. Nilijawa sana na woga alipotishia kuniua kwa risasi na majimoto. Nilipiga hatua na kuripoti katika kituo cha polisi." Alisimulia Susan.

Willy Paul amekuwa katika mapenzi mazito na mwanadada huyu kama jinsi anavyosimulia. Willy Paul alipopigiwa simu kujibu madai hayo hakuweza kushika simu yake.