Wito wa wakenya kwa Kocha Jose Mourinho kuhusu Victor Wanyama

Kufuatia kuteuliwa kwa Jose Mourinho kuwa kocha katika timu ya Tottenham Hotspur F.C, Wakenya wametoa ombi lao kwa Mourinho anapoanza kazi yake katika timu hiyo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Wakenya wamemwomba Mourinho kumrudisha Victor Wanyama kuwa miongoni mwa wachezaji 11 bora wa timu hiyo.

Victor Wanyama ambaye pia ni kapteni wa timu ya Harambee Stars hajakuwa na nafasi nzuri ya kuonesha ustadi wake katika 11 bora kwenye timu ya  Tottenham.

Jose Mourinho aliteuliwa kuwa meneja wa timu ya Tottenham Jumatano, baada ya Mauricio Pochettino kufutwa kazi Jumanne.

Mourinho ambaye awali amekuwa kocha wa Chelsea na Manchester United, amesaini mkataba mpya utakaokamilika katika kipindi cha 2022-2023.

Aidha, nduguye Victor, McDonald Mariga alicheza katika timu ya Inter Milan huku kocha akiwa Mourinho wakati huo ambapo walishinda UEFA, 2010.

Wito wa Wakenya kwa Mourinho ni kumrejesha Victor Wanyama katika nafasi ya 11 bora ili aweze kufufua makali yake ambayo yamedidimia kutokana na kusalia kama mchezaji wa akiba kila mara.

Timu ya Tottenham kwa sasa iko katika nafasi ya 14 kwenye jedwali na pointi 12 hata baada ya kucheza mechi 14.

Isitoshe, timu hiyo imekuwa na kipindi kigumu sana kwa kuwa haijawah ishinda mechi yoyote ya ugenini tangu Januari.

Soma taarifa nyingine kutoka mwaandishi: