mbusii.000.uhuru

Wolaan Rasta: Rais Kenyatta Afichua Nyimbo Tatu Anazopenda Zaidi za Bob Marley (VIDEO)

Miaka kadhaa iliopita, Rais Uhuru Kenyatta aliketi chini tena na watangazaji wa Radio Jambo Mbusii na Lion deh katika mahojiano ya moja kwa moja.

Katika mahojiano hayo, rais Kenyatta aliwafurahisha na kuwashangaza watangazaji hao alipokubali kuzungumzia upendo wake kwa muziki haswa muziki wa aina ya Reggae.

Hiyo ni baada ya mtangazaji Lion deh kumuuliza kuhusu nyimbo anazozienzi huku bwana Kenyatta akifichua kuwa yeye bado ni shabiki sugu wa muziki wake, Bob Marley, gwiji wa nyimbo za Reggae.

‘Napenda reggae kabisa lakini yangu ni ile ya zamani, mimi ni mtu ya Bob Marley” Alieleza Rais Kenyatta kabla ya kutaja nyimbo tatu za gwiji huyo wa muziki.

“Kwanza kabisa ni Stir it up, Redemption Song na Three Little Birds.” Aliongeza rais.

Ispokuwa Rais Kenyatta, Rais wa zamani wa Amerika, Barack Obama pia ni shabiki sugu wa Bob Marley na hilo lilithihirika alipotembelea nchi ya Jamaica.

Obama alitembelea jumba ambalo ni la makumbusho yake Bob Marley na kufichua kuwa hadi wa leo bado ana kanda za zamani za gwiji huyo.

Tazama kanda ifuatayo.

 

Photo Credits: victor TKO imboto

Read More:

Comments

comments