"Yaani Tanzania tumesha wai kabisa," Willy Paul

Willy-paul-696x522
Willy-paul-696x522
Staa wa muziki wa injili nchini Willy Paul ametangaza kuwa sasa ameiteka soko la muziki la nchi jirani ya Tanzania. Kupitia nyimbo alizowashirikisha wasanii Nandy na mkali Rayvany kutoka lebo ya WCB inayomilikiwa na staa mkubwa afrika Diamond Platnumz, sanaa yake imepenyeza kwa urahisi na kueleweka freshi na watanzania.

Tazama nyimbo yake hapa na Rayvanny;

Kwa utafsiri wa haraka, michambo ya wakenya katika mitandao ya kijamii huenda ilimpa nguvu staa huyu kuzidi kupambana na kujitafutia nafasi nzuri ya muziki afrika mashariki.

Pata uhondo hapa:

Willy M Tuva katika kipande kifupi cha video alichokiposti Pozze anaonekana akimpa shavu kubwa katika shoo iliyofanyika Dar Tanzania.

Tazama hapa:

https://www.instagram.com/p/ByztDE9Hjqj/

Willy Paul ni kati ya wasanii wanaopevuka kwa kasi nchini akiwemo staa wa kike Nadia Mukami, Masauti na kundi la muziki la Ochungulo. Wasanii wengi wamezungumza swala la pozze kuonekana kuasi dini na kufanya muziki wa kidunia.

Soma hapa:

"Willy paul kama anataka kufanya muziki wa kidunia yupo huru. Ni uamuzi wake." alisema HopeKid.

Staa wa muziki kutoka nchi ya Jamaica Alaine alimtetea Willy paul juzi kati kipindi na ambapo wakenya walikuwa  wanatokwa na povu katika mitandao ya kijamii kumhusu msanii huyu wa injili kuwa na tabia na mienendo inayokinzana na neno la mungu.

"Watu wamkosoe Willy paul kwa upole na kwa upendo. Jamani tusimkosoe kwa chuki na kwa ukali." alisema Alaine.