'Yope' Remix ya Diamond yashika kasi You Tube, Harmonize aipiga mikausho

7UAFkIBOhosimba chibu
7UAFkIBOhosimba chibu
Staa na fundi wa muziki Afrika Diamond Platnumz amelidondosha ligoma hatari hapo jana linalokwenda kwa jina Yope Remix akimshirikisha staa wa Kongo Innos'B. Ndani ya masaa 24, mkwaju huu sasa umegonga views Milioni moja na ushei.

Sio mara ya kwanza ngoma za Diamond Platnumz kupata utazamwaji mkubwa kama ilivyoshuhudiwa. Staa aliyemkuza na kumlea Harmonize ameonekana kuipa shavu kavu ngoma hii. Hii inajiri baada ya Harmonize kukata stima za mahusiano yua karibu na bosi wake.

Hapo awali, Konde Boy alishobokea na kuposti ngoma mbili za Rayvanyy na Mbosso ilhali sasa dogo anaonekana anafanya kuonyesha ku-balance shobo na kuipiga mikausho ngoma yoyote inayotoka usafini.

Mastaa wa karibu na Diamond Platnumz tayari washasukumu mzigo huu kwenye mtandao ili Harmonize bado bado. Je, huenda ikawa Mondi alimkosea sana Harmonize kiasi cha kwamba hawezi kumsamehe? Au Huenda Harmonize anataka kupimana nguvu na bosi wake?