Rais wa Tanzania John Magufuli amewashauri wanawake wa Tanzania kuacha wazi uzazi wao na kuzaa watoto zaidi ili kuboresha uchumi wan chi hiyo ,ushauri ambao wakosoaji wanasema utazidisha hali ya umaskini .“ Mnapokuwa na idadi ya juu ya watu ,inakuwa rahisi kuboresha uchumi . hii ndio kwa sababu uchumi wa China ni mkubwa sana’ amesema Magufuli akitoa mifano ya nchi za India na Nigeria kama baadhi ya mataifa yalio na uchumi thabiti kwa ajili ya idadi kubwa ya watu .
“ Najua wale ambao wamefunga uzazi wao watanilaani sana kwa matamshi yangu .Jiachilieni wao wakitaka wajizuie kuzaa’ .Rais Magufuli aliuambia mkusanyiko wa wenyeji katika mji wa nyumbani kwake wa Chato. Tangu alipochukua maamlaka mwaka wa 2015 alichukua hatua madhubuti ya kuanzisha kampeii ya kuzidisha viwanda chini humo hatua ambayo imesaidia uchumi kuimarika kwa jumla ya asilimia 6-7 kwa mwaka .
Lakini ameshikilia kwamba ongezeko la idadi ya watanzania litasidia kupiga jeki uboreshaji wa uchumi wa taifa hilo la afrika mashariki . Tanznia inayokadiriwa kuwa na watu milioni 55 tayari imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye ongezeko la watoto wanaozaliwa huku kila mwanamke akikadiriwa kuwa na takriban watoto watano.