Zitakavyofanyiwa noti mzee za elfu, M-Pesa kukoma kuchukua Alhamisi

unnamed (3)
unnamed (3)
Maduka ya Safaricom ya M-Pesa yatakoma kuchukua noti mzee za 1,000 kuanzia Tarehe 26, Alhamisi Juma lijalo.

Hii ni kufuatia juhudi za Benki Kuu ya Kenya kuhakikisha kuwa noti mzee za 1,000 zimeacha kutumika Septemba 30.

"Safaricom haitachukua noti mzee za 1,000 baada ya tarehe 26 Alhamisi..." Hii ni kauli ya kampuni ya Safaricom iliyotolewa leo Jumamosi.

Soma hadithi nyingine:

Baada ya Septemba 30, noti mzee za 1,000 zitaacha kutumika.

Wiki mbili zilizopita, Benki Kuu ya Kenya ilitangaza kuwa kuna noti mpya za 1,000 za kutosha .

Aidha, iliwataka wakenya kuchukua nafasi hii wabadilishe noti hizo katika benki.

Takriban noti Milioni 100 zimerudishwa katika Benki Kuu ya Kenya mwisho wa Agosti.

Soma hadithi nyingine:

Hii inaashiria kuwa asilimia 50 ya noti hizi zimerudishwa katika benki.

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Patrick Njoroge amewaomba wakenya wawakumbushe wakongwe katika jamii wawajibike katika zoezi hilo.

“Wamama , nyanya wetu wanapenda kuwekeza sana. Kuna uwezekano wana noti hizi mzee nyumbani." Njoroge alichapisha ujumbe kwa Twitter.

Noti hizi zikifikishwa katika tawi za Benki Kuu ya Kenya, zitasafirishwa katika lori hadi kwenye makao makuu.

Soma hadithi nyingine:

Zitapokelewa, kukaguliwa na baadae kuwekwa katika chumba kisicho na oksijeni chini ya ulinzi mkali.

Maafisa wakubwa watapanga siku na ambayo watakusanya noti zote.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, notihizi mzee zinakatwakatwa katika vipande vidogo na baadaye kuchomwa hadi ziwe jivu katika eneo la Kariobangi jijini Nairobi.