3 wafariki katika ajali ya barabarani

Watu watatu walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa, kutokana na ajali ya barabarani kwenye barabara ya Wamunyu-Machakos.

Naibu OCPD wa Mwala Ronald Kirui alisema kwamba watu wawili walifariki papo hapo huku mtu wa tatu akiaga alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Masii Level 4

Ajali hiyo ya Jumamosi ilitokea pale matatu ya abiria 14 iliyokuwa ikielekea Machakos ilibingiria mara kadhaa kilomita mbili kutoka mji wa Wamuyu baada gurudumu lake kupasuka.

Wengi wa waliolazwa wanauguza majeraha ya kuvunjika sehemu mbali mbali za mwili.