Afisa wa polisi wa kike auawa nyumbani kwake Eldoret

Afisa wa polisi wa kike amepatikana ameuawa ndani ya nyumba yake aliyokuwa amekodisha huko mtaa wa Jamboni mjini Eldoret. Polisi wanadai kuwa Robina Moraa alidungwa kisu na mpenzi wake ambaye sasa anatafutwa juu ya mauaji hayo.

Johnstone Ipara ambaye ni kamanda wa polisi katika kaunti hiyo ya Uasin Gishu alisema afisa huyo wa kike alidungwa kisu kifuani na pia tumboni huku mwili wake ukipatikana katika dimbwi la damu.
Kamanda huyo aliongeza kuwa Moraa ambaye alikuwa anafanya kazi katika maeneo ya mashariki ya mji wa Eldoret, alionekana mwisho katika kampuni ya mchumba wake kabla ya mwili wake kupatikana mapema leo.

Mwili huo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Moi Refferal.