Ahmed Khalid alikosa kusafiri na ndege ya Ethiopian iliyofanya ajali

Ahmed Khalid anahesabu bahati ya maisha yake kwa kukosa kusafiri na ndege ya Ethipian ya ET 302 iliyofanya ajali Juma pili baada ya kung'oa nanga.

Ndege hiyo iliweza kuanguka baada ya dadika sita, ilisababisha vifo vya watu 157, huku nchi ya Kenya ikipata mpigo mkubwa kwa kuwapoteza wananchi 32 katika ajali hiyo.

Kulingana na TRT Ahmed aliweza kukosa kusafiri na ndege hiyo ya Ethiopian ya aina ya ET 302 kwa kucheleshwa na ndege ya Dubai iliyokuwa inakuja Addis ili aweze kupanda ET 302 imlete hadi Nairobi.

Ilimbidi angoje ndege ya kutoka uwanja wa ndege wa Bole iliyotua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta siku baada ya ajali hiyo.

Ilikuwa ni bahati na baraka kwa Ahmed kwa kukosa ndege hiyo iliokuwa inatoka Addis-Ababa kuelekea uwanja wa Jomo Kenyatta Nairobi.

Ni nchi mbalimbali zilizoomboleza kisa hicho, huku UN ikiamua kufunga bendera 193 milingoti nusu ili kuwaomboleza wafanyakazi walioangamia kutokana na ajali.

Juma pili wingu jeusi liliweza kutanda nchini Kenya kwa habari hizo za kuhuzunisha, ndege hiyo iliweza kuuwa watu na pia wafanyakazi wa ndege hiyo.

Akiongea kuhusu kuepuka kwake kwa ajali hiyo alisema..

" Kwa sababu ya kucheleshwa na ndege ya Dubai, nilikosa ndege ya kwanza ya kuja Nairobi abiria mmoja aliona katika simu yake kuwa ndege ya kwanza ishaa ng'oa nanga kwa muda wa dakika sita,

"Kisha akaona baadaye imeweza kufanya ajali," Alisimulia Ahmed.

Ni wasiwasi uliowapata jamaa za wasafiri waliokuwa katika ndege hiyo huku wakiweza kushauriwa wawe watulivu na kuambiwa kuwa watapewa habari zaidi kuhusu ajali hiyo.

Wananchi waliweza kuandika rambirambi zao katika mitandao ya kijamii, huku bado jambo lililo sababisha ajali hiyo haikubainika na uchunguzi kuendelea zaidi.

Ahmed aliweza kuwasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Jumatatu akiwa mzima na kisha kupokelewa na familia yake iliyokuwa inamgonja katika uwanja huo.