Aki wewe ni husband material from heaven! Diana ajibu Bahati kuhusiana na harusi ya kifalme

NA NICKSON TOSI

Diana Marua hatimaye amejibu madai ya mpenziwe Bahati kuhusiana na tamko kuwa atandaa harusi kubwa na ya kifahari ambayo macho ya wakenya hayajawahi kuona kamwe ikifanyika nchini.

Wachumba hao wawili wamekuwa wakiishi pamoja kwa muda sasa takriban miaka 3 na wamejaliwa watoto 2 Majesty na Heaven .

Diana kama njia ya kujibu ujumbe wa Bahati kuhusiana na harusi yao aliandika hivi, japo maandishi yake tumeyaeweka katika lugha ya Kiingerza.

”My hubby, my best half, best friend, heartbeat, sunshine, ride or die, my soulmate, The one who God chose for me. I am thankful to God for you, you are a blessing in my life,”aliandika Diana.

Diana alimaliza ujumbe kwa kumuambia mpenzi wake Bahati kuwa anatazamia kushuhudia harusi hiyo jinsi alivyoandika Bahati katika mtandao wake wa Instagram

Hapa ni maandishi yake Diana.

”Tumetekeleza vitu vingi sana tukiwa pamoja ,napenda jinsi unavyojituma na ili kukimu maisha yetu na nashukuru kwa yale yote ambayo umetufanyia kama familia yako .Najua mambo mapya na makuu yapo njiani yaja na siwezi kosa kuyaona.Aliandika Diana.

Bahati na Diana wanafahamika sana kutokana na maisha yao ya kifahari wanayoishi na sasa wengi wanatarajia kushuhudia harusi baada ya janga hili la Corona likitulizwa.