Alikiba afichua siri waliyozungumzia na mke wake Amina

ali kiba
ali kiba

Ali Kiba alifunguka na kusema walichozungumzia mara ya mwisho aliongea na mke wake, Amina Khalef.

Habari za waapenzi hawa zimekuwa zikisambaa kama moto nyikani kuhusu matatizo wanayokumbana nayo katika ndoa yao.

Mwanamziki huyu wa nyimbo za Bongo alisema kuwa, anajaribu kurekebisha uhusiano wake na mke wake.

Akizungumza na waandishi wa Tanzania, katika kipindi cha Shilawadu, alisema kuwa, mke wake yupo karibu kujifungua mtoto wao wa pili.

Zaidi ya hayo, Ali Kiba alisema kuwa, bado mke wake hajajifungua na kwa bahati mbaya au nzuri bado hawajaangalia kama mtoto wao ni wa kike au wa kiume.
“I CALLED HER, WE TALKED ABOUT MANY THINGS. MY WIFE HAS NOT YET DELIVERED AND BY GOOD OR BAD LUCK, WE HAVE NOT CHECKED IF IT IS A BOY OR A GIRL.” Alisema.

Ali Kiba alipoulizwa anatarajia mtoto wa jinsia ipi, alisema kuwa, hawezi chagua kwani mtoto ni mtoto.

I AM OKAY WITH ANY GENDER THAT GOD WILL GIVE US.

Mtoto wa kwanza wa wapenzi  hawa alizaliwa mwaka uliopita na jina lake ni  Sheikh Keyaan.