Viroja!Alikuwa na maiti iliokuwa inampa pesa-yaya wa pangani afichuwa siri ya mwajiri wake

Ni ndoto ya kila msichana kusoma hadi chuo kikuu na kupata ajira kujikimu kimaisha, lakini kwa Penninah Awuor ilikuwa kitendawili kwake kutojuwa kuwa siku moja atakuwa mfanyikazi wa nyumbani au yaya.

Awuor amefanyia watu wengi kazi ya nyumba na kupitia mateso mengi akiwa mikononi mwa wajiri wake.

Baada ya kuja Nairobi eneo la Pangani alipata kazi ya nyuma na kufikiri kuwa ataendeleza maisha yake na ya ndugu zake lakini hakujua ni kazi mbaya ambayo hangetaka kufanya maishani mwake.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini alieleza jinsi alipatana na mwajiri wake anayefahamika kama Mohammed Abdi Noor.

Mbali na kazi yake ya kawaida Awuor alieleza jinsi alilazimishwa kusafisha maiti.

"Nilipofika katika nyumba Mohammed hakuwepo, nilipata mkewe na akanipa majukumu yangu, lakini aliniambia ningoje mume wake aje ili anionyeshe kazi nyingine ya kufanya.

Mumwe alipofika walinipeleka katika chumba kimoja na kuniambia nivute kitanda kilicho kuwa chumbani humo. 

Nilishtuka nilipoona maiti imefungwa ndani ya mkeka, niliogopa na kushtuka, akaniambia nisishtuke." Alisimulia Awuor.

Mkewe Mohammed ambaye alikuwa amesimama kwa mlango akiwa ameshika bunduki alimweleza jinsi ya kuosha maiti.

" Weka kitambaa katika maji moto lakini si moto kabisa, osha maiti huyo kama vile dirisha huoshwa, alinilazimisha kulala na maiti huyo lakini nilikataa." Alisema.

Mfanyakazi huyo hakuwa na lolote la kufanya ama popote pa kuenda ila kufuata maagizo aliyopewa na mwajiri wake.

Baada ya kuonyeshwa familia yote alianza kazi lakini alikuwa amesongwa na mawazo tele, huku akisalia tu maombi.

Penninah alikuwa anaomba kimoyomoyo ili mwajiri wake asiweze kumsikia, alieleza jinsi maiti hiyo ilikuwa inatoa pesa.

" Baada ya kuosha maiti hiyo saa nne kamili, mwajiri wangu alikuwa anarudi nyumbani mwendo wa saa nane akitoka kazini mwake eneo la Eastleigh 

Ningetoa maitu hiyo alikokuwa amefichwa na kuanza kutoa pesa kuanzia 500 na 1000 pesa hizo zilikuwa mpya." Alieleza.

Alipewa ilani na mkewe Mohammed asiwahi chukua pesa kwa hiyo nyumba bila ruhusa yao.

"Aliniambia nisiwahi chukua pesa kwa hiyo nyumba bila ruhusa yao, kwa sababu naweza beba laana ama niwe wazimu." Alisema.

Akiongeza,

"Kuna daktari ambaye alikuwa anakuja kila jumanne na ijumaa kudunga maiti hiyo sindano, baada ya hapo Mohammed angemvalisha kanzu na kofia 

Siku moja daktari alipotoka aliniambia maiti anataka kushiriki ngono. nmeosha maiti kwa siku arobaini na nmeajiriwa kwa siku,47." Awuor Alinena.

Yote tisa kumi ni,

"Usiku huo mkewe alisikia kelele hapo ndipo alikuja na kuniuliza kilichotokea, nikamwambia kila kitu lakini alinichapa, baadaye Mohammed alikuja na kunipa kichapo cha mbwa

Alinifukuza nikalala na bawabu hadi asubuhi, kesho yake nilienda katika kituo cha polisi kuripoti kitendo hicho lakini hakuna haki ambayo ilitendeka." Alisema  Awuor.

Cha kushangaza ni kuwa Awuor hajawahi lipwa siku hizo,47 je haki za waajiriwa nchini zinazingatiwa kweli?.