Barua ghushi ya kuua Ruto, Dennis Itumbi akabiliwa na mashtaka mapya

Dennis Itumbi
Dennis Itumbi
Mwanastratejia wa kidijitali Dennis Itumbi na shahidi Samuel Gateri wamekabiliwa na mashtaka mapya katika kesi wanayohusishwa ya kuandika barua ghushi iliyosheheni njama ya kumuua naibu wa rais William Ruto.

Wawili hawa wamekabiliwa na mashtaka haya leo Jumanne baada ya upande wa mashtaka kukusanya ushahidi wa kesi zinazowakabili.

Dennis na Samuel walikana mashtaka ya kuchapisha barua ya uongo inayokinzana na sheria.

Tuhuma za kuandika barua ya Mei, 30 2019 zinawaandama.

Kesi hii itasikilizwa Novemba 18.

Mwezi jana, Gateri alihukumiwa na kuachiliwa kwa dhamana ya elfu 100,000.

 Gateri alihukumiwa katika mahakama ya Milimani kwa kuandika barua pasi na misingi yoyote ya kisheria.

Barua hii ghushi ya Mei 30 ilidaiwa kuwa na sahihi ya waziri na ilijaa njama ya kumtoa uhai Ruto.

Vilevile, ameshtakiwa kwa kuchapisha kauli ya uongo inayolenga kuzua mtafaruku kwa umma.

Gateri alikana madai haya mbele ya hakimu Francis Andayi na kuachiliwa kwa dhamana.