Bintoye huyo wa kiongozi wa ODM Raila Odinga ameanza kurejelea maisha ya kawaida na amechapisha msururu wa picha zake akiwa katika sehemu mbali mbali katika maisha ya kawaida baada ya kukimya katika mitandao ya kijamii kwa miaka minne . Mama huyo ya watoto wawili aliweka picha katika instagram huku moja ikiwa na ujumbe
“stronger than ever.”
Baadhi ya maoni katika posti hiyo iliwoanyesha wengi wanaomshabikia wakiwa na furaka kujua kwamba Rosemary amerejea kwa njia thabiti
carolradull Oh my baby
mongsderr Long time no see
miss.amolo Love the tee
judy_onserio I thank God for your health
evancewashingtonejuma That’s the Spirit my good friend. Always here for you.
Picha yake ya mwisho alioiweka instagram ilikuwa yake na Jalang’o mwaka wa 2016 Novemba muda mfupi kabla ya kuanza matibabu baada ya kupofuka . Tatizo lake la macho lilianza mwaka wa 2017 alipozirai muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa mafunzo ya wanawake kisha akakimbizwa hospitalini kwa ambulansi .
Baadaye alisimulia jinsi alivyokuwa na maumivu makali ya kichwa lakini akapuuza ,baadaye alipatikana kuwa na uvimbe katika ubongo wake na hata akajipata katik coma . Baadaye kaika mahojiano babake Raila alisimulia jinsi kundi la madaktari 10 wa China walivyoweza kuokoa maisha yake katika upasuaji uliodumu kwa saa 10 katika chuo kikuu cha Peking .
Waziri huyo mkuu wa zamani amesema maisha ya binti yake yaliokolewa China baada ya miezi mitatu ya matibabu afrika kusini na Israel bila mafanikio.Odinga pia amefichua kwamba Rosemary alianza kuona baada ya kutumia matibabu ya dawa za kiasili kutoka India .