safaricom1

Bob Collymore hatari wa ku-rap ! Afanya majanga kwenye ” Furi Furi”( Video)

Kama kweli kifo sio rafiki wa binadamu. Hii leo nchi nzima imeamkia ripoti za tanzia kuwa mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom amefariki kutokana gongwa hatari la saratani. Bob amekuwa akiugua ugonjwa huu kwa miaka kibao.

Soma hapa pia:

Tanzia! Tazama jinsi Akothee, King Kaka walivyomuomboleza Bob Collymore

Bob alikuwa mjasiriamali na mwenye falsafa ya kusonga mbali zaidi. Aliweza kuiweka kampuni ya Safaricom katika ramani nzuri katika ushindani wa kampuni za mawasiliano duniani.

Ila je, ulikuwa na ufahamu kuwa kiongozi huyu alikuwa na uwezo wa kuchana katika wimbo? Msanii wa nyimbo za injili Jimmy Gait alipata nafasi ya kumshirikisha katika wimbo wa Furi Furi.  Mastaa wengine waliokuwa katika nyimbo hii ni Julie Gichuru, Jeff Koinange and Coccoh.

Soma hapa pia:

Soma ujumbe wa mwisho wa Bob Collymore. Risala za viongozi na mastaa

 Bob aliupenda muziki sana katika maisha yake. Tazama jinsi alivyoweza kuchana vipande hatari katika video hii:

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments