Bonge la parte! Diamond na Tanasha wampa mwanao sherehe ya kufana (PICHA)

Picha za sherehe ya mwana wa Diamond Platnumz na Tanasha zaacha wengi vinywa wazi

Bara la Afrika na sana sana ukanda huu wa mashariki, jambo linalozungumziwa kwa sasa ni sherehe za kishua za mwanawe, staa wa Bongo, Diamond Platnumz na mkewe Tanasha Donna.

Sherehe hizo ambazo ziliandaliwa katika jumba la kifahari la Diamond, Madale katika mji mkuu wa Dar es Salaam, zilikuwa za kusheherekea siku 40 tangia kuzaliwa kwa mwanao, Naseeb Junior.

Wawili hao walichukua fursa hiyo ya kipekee kuonesha uso wa mwanao kwa mara ya kwanza tangu kuzaliwa kwake.

Sherehe hiyo ya kipekee, ilikuwa na watu mashuhuri wakiwemo wanachama au wanakundi wa Wasafi, familia ya Diamond ila hamna yeyote  kutoka familia ya Tanasha aliyehudhuria.

Maadhimisho ya siku 40 ni kawaida katika tamaduni za Kiislamu kwa mama kupumzika baada ya kujifungua kwa siku 40.

Mama hapaswi kufanya chochote isipokuwa kumtunza mtoto mchanga; jamaa na marafiki huja kumsaidia. Mama huchukua majukumu yake ya nyumbani tena na huonekana nje ya nyumba siku ya 40 wakati sherehe hiyo ilifanyika.

Ziara ya ufuatiliaji imepangwa kwa siku hii ili ziara hiyo iweze kuingizwa kwenye sherehe. Ziara hiyo ina madhumuni 3:

1) Kuhakikishia afya ya mama; 2).

Kuangalia afya ya mtoto 3.

Kusaidia mama na uzazi.