Boni Khalwale ahamia rasmi chama cha Ford Kenya

Aliyekuwa seneta wa kakamega Boni Khalwale ambaye pia ni naibu kinara wa chama cha ford Kenya amehamia rasmi katika chama cha jubilee

Khalwale ambaye amekaribishwa jubilee na naibu wa rais William ruto amesema chama chake cha ford Kenya hakiwezi kuwasaidia waluhya kuingia serikalini.

Kwingineko

Afisa wa ukaguzi wa madini katika ofisi za mpakani eneo la Taveta, kaunti ya Taita Taveta Godfrey Nyamai amewatahadharisha wachimbaji madini dhidi ya kutumia njia za mkato ili kupata vilipuzi vya kutumia timboni.

Anasema kando na hatua hiyo kuwa uvujaji wa sheria, huenda watakabiliwa na shtaka la kubeba au kutumia vilipuzi hivyo bila kibali.