efebqxupqj925df0c24c7ed0e-compressed

Bosi awatuza wafanyikazi 200, milioni 50 kila mmoja za Krismasi

Kampuni moja ya kuuza majumba imewashangaza wafanyikazi wake wakati huu wa Krismasi kwa kuwazawidi tuzo ambayo hawakutarajia.
Wakati msimamizi wa kampuni ya Maryland alipowapa bahasha nyekundu wafanyakazi wake katika sherehe ya likizo ya Krismasi, wengi wao hawakufahamu thamani ya zawadi iliyokuwa ndani.
Wafanyikazi hao 200 walituzwa shilingi milioni 50 kila mmoja kama zawadi kwa kazi njema kutoka msimamizi wa kampuni hiyo.
Jumla ya kima cha fedha waliyopata wote ni zaidi ya bilioni moja.
“Nilipofungua bahasha yangu, sikuamini macho yangu,” Stephanie Rdigway ambaye ni naibu maneje wa utendakazi aliiambia kituo cha habari cha CNN.
“Sikuamini niliona kile nilichoona. Sina misamiati ya kuelezea jinsi ninavyohisi, ninafuraha sana, ni maajabu.”
Kulingana na mahojiano na CNN msimamizi mkuu wa kampuni ya St. John Properties, Lawrenze Maykrantz alisema kuwa walitoa shukran kwao baada ya kampuni hiyo kuaafikia maazimio yao ya mwaka huu.
“Tulitaka kufanya jambo la kuwashukuru wafanyi kazi wetu kwa kutimiza malengo ya kampuni, na tulitaka kuwapa kitu kikubwa,” Maykrantz alisema.
Aidha aliongeza kusema kuwa kila mwajiriwa alipata bonasi hiyo kulingana na miaka aliyohudumu katika kampuni hiyo.
Kiwango kidogo zaidi alichopata mwajiriwa ambaye hata hajaanza kazi ni shilingi  elfu 10,168 huku shilingi milioni 27,453,600 ukiwa mgao mkubwa zaidi.
“Ni kweli hili ni jambo la furaha sana ambalo sijawaishuhudia katika maisha yangu. Kila mmoja amefurahi sana. Walishangilia, wakalia,wakacheka na hatakukumbatiana,”
Kampuni hiyo ya St. John Properties ambao ina matawi manane, kwa mara ya kwanza iliwalipia wafanyakazi wake tiketi za ndege pamoja na ada za hoteli kwenye sherehe ya kufunga mwaka.

Photo Credits: CNN

Read More:

Comments

comments